May 7, 2016


Mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Mwadui FC ni kesho na inasubiriwa kwa hamu ile mbaya. Itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Lakini kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema atahakikisha anashinda mchezo huo ili Yanga iwe bingwa.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 68 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 58, wakati Azam ina pointi 57. Yanga na Azam zimebakiwa na michezo mitatu, huku Simba wakiwa nayo minne.

Simba ikishinda mechi zake zote ikiwemo hii na Mwadui, itafikisha pointi 70, hivyo Yanga na Azam zikipoteza mechi zake zilizobaki, Wekundu wa Msimbazi wanaweza kuwa mabingwa.

Julio ambaye amewahi kucheza na kufundisha Simba, alisema hataleta urafiki kwenye mchezo huo na amepanga kushinda ili Yanga ipate ubingwa rasmi.

“Siwezi kusema niache kumfunga Simba kisa tu Yanga asiwe bingwa, mimi naiandaa timu yangu kushinda na nataka niwafunge Simba.

“Sina haja ya kuwaachia ili kuichelewesha Yanga kuwa bingwa, kama bingwa anajulikana nani anaenda kuwa bingwa, acha niwafunge tu,” alisema Julio ambaye timu yake ipo nafasi ya sita na pointi 37.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV