May 12, 2016


Yanga inatarajia kuondoka nchini Jumapili alfajiri kwa safari yake ya kwenda Angola kuwavaa Esperanca.

Mechi kati ya Yanga dhidi ya wapinzani wao itachezwa Jumatano ijayo.

Katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho iliyochezwa jijini Dar es Salaam, Yanga ilishinda kwa mabao 2-0.
Kikosi cha Yanga kitaondoka na ndege ya kukodi, ingawa bado haijajulikana idadi ya watakaoongozana nayo.


“Kama ndege itakuwa kubwa, basi tutaondoka na watu wengi zaidi. Kama itakuwa ndege ndogo tutakuwa na idadi ndogo ya watu,” alisema Msemaji wa Yanga, Jerry Muro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV