May 12, 2016


Uongozi wa Yanga umesema haitakuwa sawa watu kuandaa matamasha kwa kisingizio cha kuipongeza timu kwa kubeba ubingwa.

Mkurugenzi wa kitengo cha habari cha Yanga, Jerry Muro amesema utengenezaji wa fulana au kuandaa matamasha hauwezi kuwa sawa.

"Hauwezi kuwa sawa bila ya baraka za uongozi, anayetaka kutengeneza fulana au kuandaa tamasha basi afike ofisini na kuwasiliana na uongozi.

"Kila kitu ndani ya klabu kubwa kama Yanga kinakwenda kwa mpangilio, haiwezi kuwa sahihi kila mmoja afanye anachotaka yeye," alisema Muro.

Mara baada ya Yanga kutwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo, kumejitokeza makundi ya mashabiki wa Yanga ambao wamekuwa wakitengeneza fulana zao zenye maandishi mbalimbali ya kuisifia timu hiyo na kuipongeza kwa kubeba ubingwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV