June 26, 2016


Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali ameibuka na kusema kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linapaswa kubadilishwa jina na kubadikwa lile la ushabiki wa TP Mazembe.

Akilimali amesema pamoja na kelele nyingi za TFF kutaka kuonyesha Yanga haijui sheria lakini kuna njama za kila aina zimekuwa zikifanywa kutaka kuiangusha Yanga.

Kiongozi huyo wa wazee wa Yanga ameishutumu TFF kuingia kwenye mtandao wa Caf na kupanga tarehe bila kuiambia Yanga halafu ikatangaza kwamba Yanga walichelewa.

“Yanga walichelewa? Kama TFF ni ya Tanzania vipi haikuzungumza na Yanga na kuwaeleza hilo? Hapa kuna kitu cha ajabu kabisa, TFF wanaweza vipi kupanga tarehe bwana halafu waseme Caf.

“Tena Yanga ilitaka mechi ichezwe baada ya watu kufuturu. Lakini kwa kuwa wanajua muda huo, kwenye TV kutakuwa na taarifa ya habari, basi wakaamua kuipangia Yanga icheze mchana.

“Sasa hapa unaangalia maslahi ya Yanga au ya TV. Kweli hii si haki na hiki ndiyo chanzo cha TFF kuihujumu Yanga kwa kuwa inataka watu wengine wafaidike,” alisema Akilimali na kuongeza.

“Wanasema Caf ndiyo wana haki ya matangazo ya TV, sawa. TBC wana uwezo pia, vipi hawakutoa nafasi, huenda wangeweza kulipa fedha nyingi zaidi kwa Caf.

“Kwa nini wamelazimisha Azam tu, TBC ina vifaa na Wachina wamewapa vifaa vipya kabisa hivi karibuni.

“Najua watu wanawaona Yanga kama hawajui, wanawaona kama vile wanapayuka. Lakini ndani yake hawajui kuna nini.

“Nashangazwa sana na TFF wanavyofanya, wanashindwa kuthamini mchango wa Yanga kufikia hapa ilipo. Ndiyo inayowafanya TFF sasa wawe busy kuwasiliana na Caf na wanasikika kimataifa.

“Kwani lini mara ya mwisho timu ya Tanzania kucheza hatua hii. Hawa TFF vipi wanaonekana kama hawakufurahishwa na Yanga kufika hapo,” alihoji Akilimali.

Yanga imekuwa katika malumbano makubwa na TFF huku ikidai shirikisho hilo limekuwa likifanya mambo bila ya kufuata utaratibu.

Lakini TFF imekuwa ikisisitiza kuwa Yanga hawakujifunza mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na kutokwenda kwenye semina ya Caf wakati wa upangaji ratiba.


Lakini kuhusiana na hilo, Akilimali anasema: “Hao TFF nimesikia nao walitakiwa kwenda kwenye semina pia hawakwenda. Sasa kwa upande wa Yanga wanshupalia kwelikweli. Kawaulize, vipi hawakwenda kwenye semina, huenda nao kuna mambo mengi hawajui.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV