June 26, 2016

NAPE

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye amewaeleza wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys kwamba wameonyesha soka safi.

Nape alikuwa uwanjani wakati taifa Stars ikipambana na Shelisheli na kuwachapa kwa mabao 3-0 katika mechi ya kuwania kucheza michuano ya Afrika.

“Kweli mmeonyesha soka safi, soka la kuvutia na kujituma. Niwaambie sisi kama serikali tumevutia na mlichokifanya.

“Matumaini yetu kama mtaendelea hivi ni kulisaidia taifa letu,” alisema.

Serengeti Boys ilionyesha soka la kuvutia na kuipa wakati mgumu Shelisheli.

Hata hivyo, Serengeti Boys watalazimika kuwavaa vijana Shelisheli kwa mara ya pili na kama watafuzu watakutana na Afrika Kusini ili kupata nafasi ya kuwania kucheza michuano ya Afrika itakayofanyika mwakani nchini Madagascar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV