June 29, 2016


Straikawa zamani wa Ndanda FC, Atupele Green, ametoa siri iliyosababisha agome kujiunga na Simba na kuamua kutua kwa ‘Wajeda’, JKT Ruvu.

Atupele amejiunga na timu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu.

Mshambuliaji huyo aliyemaliza ligi akiwa na mabao 10, alikuwa akitajwa kutakiwa na Simba na Azam FC lakini zote amezipiga chini na kujiunga na timu hiyo huku sababu kubwa ikiwa ni kuonekana ni mamluki.

Atupele amesema kuwa Simba ni miongoni mwa timu zilizokuwa zikimhitaji lakini aliamua kuachana nao kufuatia madai ya kuwa ni shabiki wa Yanga.

"Kweli Simba walikuwa wakinihitaji na mazungumzo  walishaanza kupitia wakala wangu lakini katika mazungumzo hayo nikasikia kutoka kwao kuwa wanasema mimi ni Yanga kutokana na kucheza timu ya vijana ya Yanga.


"Baada ya kuona hivyo, nikaamua kuachana nao na kujiunga na JKT kwa sababu  kazi yangu ni soka sasa inapotokea watu wanazusha maneno ambayo hayana ukweli ni bora kuachana nao kwani mwisho wake ni kukupoteza kimpira kitu ambacho sitaki kitokee kwangu," alisema Atupele.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV