June 7, 2016Beki mpya wa Yanga, Andrew Vicent ‘Dante’ ana wazimu wa kupenda wanyama ile mbaya.

Dante ambaye amejiunga na Yanga akitokea Mtibwa Sugar, amesema anapenda sana kuwa mfugaji.

“Kweli ninapenda sana masuala ya mifugo, napenda kufuga wanyama wa aina mbalimbali.“Ukija nyumbani unaweza kuthibitisha hilo. Mbwa pia wapo, ninawapenda sana, tena sana,” alisema.

Dante ni kati ya mabeki wabishi nchini na Yanga imeamua kuimarisha kikosi chake zaidi kwa kuimarisha ukuta wake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV