June 26, 2016


Uongozi wa Yanga umeamua mechi yao dhidi ya TP Mazembe keshokutwa Jumanne itakuwa bure.

Mashabiki wataingia bila kulipa kiingilio kushuhudia mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Imeelezwa, uamuzi huo umepitishwa usiku huu baada ya viongozi wa Yanga kukutana katika kikao cha pamoja na Mwenyekiti, Yusuf Manji.

"Kikao ni kati ya baadhi ya viongozi pamoja na mwenyekiti. Uamuzi ni kwamba mechi hiyo itakuwa haina kiingilio na mashabiki waaruhusiwa kwenda kwa wingi kuishangilia Yanga," kilieleza chanzo.

"Si lazima kila shabiki anayekuja awe wa Yanga, waambie na mashabiki wa Simba waje. Hata kama watabeba bendera tu za Tanzania. 

"Yanga ni ya Tanzania, Yanga haitokei Congo na TP Mazembe haitokei Tanzania, waje waishangilie timu ya Tanzania."

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV