June 27, 2016


Mkuu wa kitengo cha habari cha klabu ya Yanga, Jerry Muro ndiye mgeni rasmi wa mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya Yanga dhidi ya TP Mazembe.

Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu, itapigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na tayari Yanga wametangaza mchezo huo ni bure, yaani mashabiki hawatalipa kiingilio.

Taarifa za ndani kutoka Yanga zinaeleza kuwa Muro ndiye atakuwa mgeni rasmi na kama kutakuwa na mgeni kutoka serikalini, Muro atabaki kuwa mgeni rasmi upande wa Yanga.

“Kweli hilo limepitishwa, Muro atakuwa mgeni rasmi,” kilieleza chanzo cha uhakika.


Juhudi za kumpata Muro kulizungumzia suala hilo, kuligonga mwamba kwa kuwa hakupokoea simu yake ya mkononi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV