June 30, 2016


Kocha Vicente Del Bosque ameamua kuachana na Hispania baada ya timu hiyo kuvuliwa ubingwa wa Euro.

Hispania ilivuliwa ubingwa katika hatua ya 16 Bora ya michuano ya Euro baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Italia.

Del Bosque ameamua hivyo leo mchana na taarifa zikafikishwa kwa Rais wa Shirikisho la Soka la Hispania, Angel Villar.

Imeelezwa, awali Del Bosque alizungumza na raise huyo juzi Jumanne, lakini ilionekana kama hakukubaliana na uamuzi wake. Huenda kulikuwa na namna ya kutaka kumshawishi abaki.


Kocha huyo ameiwezesha Hispania kubeba ubingwa wa Kombe la Dunia na Kombe la Euro mara taut mfululizo.

Pia inaelezwa, De Bosque alimueleza raise huyo kwamba hats kama angechukua ubingwa, hakuwa na mpango wa kuendelea baada ya michuano ya Euro kwisha.


Taarifa nyingine zimesema, kuna baadhi ya masuala atakayomalizia ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa ripoti na Julai 14 ndiyo rasmi ataondoka na kuachana na kazi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV