June 30, 2016

WAWA

Mabeki wa Azam FC Shomari Kapombe na Serge Wawa wako nchini baada ya kupata matibabu nchini Afrika Kusini.

Kapombe anaendelea vizuri na anatarajia kuanza mazoezi mwezi ujao tarehe 17 na imeelezwa ataanza mazoezi ya taratibu.

Kapombe alikuwa akisumbuliwa na tatizo la mfumo wa kusukuma damu na linaonekana kupona haraka na mategemeo ni makubwa.

KAPOMBE AKIPAMBANA....

Lakini Wawa raia wa Ivory Coast ambaye amekuwa akisumbuliwa na magoti, naye anatakiwa angalau kuwa na mapumziko ya muda wa zaidi ya mwezi mmoja.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga amesema wana faraja kubwa kutokana na matibabu ya wachezaji hao kuwa na mafanikio.


“Inaonekana wanaendelea vizuri kupitia matibabu hayo ya Afrika Kusini na sasa wanaendelea na tiba likiwemo hilo suala la Wawa kutakiwa kupumzika,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV