June 25, 2016


Baada ya Yanga kuandika barua kwa Shirikisho la SokaTanzania (TFF), kuomba ipate nafasi ya kumtumia Hassan Kessy, Simba wamelizungumzia suala hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema jeuri ndiyo iliwaponza Yanga hadi suala kufikia lililopo sasa, hivyo wanatakiwa kubadilika na kuwa waungwana na kuachana na majivuno.

Hans Poppe 'raia' wa Iringa, amesema kama Yanga wanataka kumtumia Kessy, waandike barua na iwe ya kiungwana, nao watajibiwa kiungwana.

"Sisi ni waungwana kweli, lakini kama mtu atakuwa anaonyesha dharau, anasema yeye ni timu ya wananchi basi tuone itakuwaje.

"Lakini kama ni muungwana, basi anajibiwa kiungwana. Wao waandike barua na sisi tutaona iko vipi. Kama wataandika na barua itaonekana si ya kiungwana, basi wasubiri kumtumia baadaye baada ya pingamizi za usajili kupita," alisema Hans Poppe ambaye ni mwanajeshi mstaafu.

Yanga ilishindwa kumtumia Kessy katika mechi yake dhidi ya Mo Bejaia nchini Algeria baada ya blog hii kuandika kwamba kulikuwa na tatizo.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas amesema kweli Yanga wameishawasilisha barua hiyo na wanategemea uungwana wa Simba kulimaliza hilo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic