June 25, 2016


Yanga imeandika barua kwa Shirikisho la SokaTanzania (TFF), kuomba ipate nafasi ya kumtumia Hassan Kessy katika michuano ya Kombe la Shirikisho, wakianza na mechi dhidi ya TP Mazembe, Jumanne ijayo.

Kessy alikuwa ndiyo anamaliza mkataba na Simba, wakamsajili, mara moja akaanza mazoezi hadi kupelekwa Uturuki kuanza mazoezi.

Lakini Yanga ilishindwa kumtumia Kessy katika mechi yake dhidi ya Mo Bejaia nchini Algeria baada ya blog hii kuandika kwamba kulikuwa na tatizo.

Baada ya hapo, baadhi ya mashabiki wasiojua wa Yanga walilaumu kuhusiana na blog hii kuandika wakidai inawahujumu.
Lakini baadhi ya viongozi wa Yanga wanaojua masuala ya soka, walilifanyia kazi na kugundua kuna walakini kweli.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas amesema kweli Yanga wameishawasilisha barua hiyo na wanategemea uungwana wa Simba kulimaliza hilo.


“Uungwana wa Simba ndiyo utakaolimaliza suala hilo, tunasubiri,” alisema Mapunda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV