June 13, 2016


Graziano Pelle amefunga bao katika dakika za nyongeza za mchezo na kuipa uhakika wa ushindi Italia ambayo imeichapa Ubelgiji kwa mabao 2-0 katika mechi yao ya kwanza ya Euro 2016.

Kabla ya hapo, Giaccherini alikuwa ametikisa nyavu za Ubelgiji katika kipindi cha kwanza.

Nahodha Eden Hazard na mpachika mabao wa Everton, Romelu Lukaku walionekana kufanya kila juhudi kupata bao, lakini ilishindikana hadi Pelle anayekipiga Southampton alipomaliza kazi kabisa. 

Belgium XI: Courtois, Ciman, Alderweireld, Vermaelen, Vertonghen, Nainggolan, Witsel, De Bruyne, Fellaini, Hazard, Romelu Lukaku.
Subs: Mignolet, Carrasco, Mertens, Denayer, Meunier, Origi,Kabasele, Dembele, Benteke, Jordan Lukaku, Batshuayi, Gillet.
Italy XI: Buffon, Barzagli, Bonucci, Chiellini, Candreva, Parolo, De Rossi, Giaccherini, Darmian, Pelle, Eder
Subs: Sirigu, De Sciglio, Ogbonna, Zaza, Florenzi, Thiago Motta, Immobile, Sturaro, Insigne, Bernardeschi, El Shaarawy, Marchetti.
Referee: Mark Clattenburg (England)
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV