June 14, 2016
Yanga imeanza mazoezi yake ya kujiandaa na mechi dhidi ya Mo Bejaia, safari hii yakifanyika usiku hadi saa sita.

Uamuzi wa Kocha Hans van der Pluijm ni kufanya mazoezi kwa kipindi hicho ili kuendana na wakati ambao mechi itachezwa nchini Algeria.

Kocha Pluijm amekuwa akiwafua vijana wake usiku kwa kuwa kinakuwa ni kipindi chenye baridi.

“Huo ndiyo wakati ambao mechi itachezwa, ndiyo maana kocha anafanya mazoezi kipindi hicho,” alisema mmoja wa maofisa walioongozana na timu.


Yanga imeweka kambi mjini Antalya, Uturuki umbali wa mwendo wa saa 1 na dekika 20 kwa ndege kutoka jiji kubwa zaidi nchini humo la Istanbul.

1 COMMENTS:

  1. Kaka Salehe hebu jaribu basi siku moja kutupa walau uchambuzi wa team pinzani ya kule Algeria itakayocheza na yanga.Fanya individual analysis na pia fanya team analysis na fananisha na Yanga. Ili hata mashabiki wapate uaelewa walau kidogo wa hali halisi. hI MIPICHA MIZURI UNAYOITUMA HAITUSAIDII KUJUA. Ila inatufanya tuvimbe vichwa mwisho wa siku tunaenda kupigwa bao tunarudi vichwa chini.Maana picha hizi za hoteli nzuri, bwawa la kuogeleaa ni kama vile yanga itachezea mechi pale kwenye bwawa la hotel na kushinda....waandishi wa habari mna nafasi kubwa sana ya kusaidia wachezaji wajitambue na pia kusaidia washabiki wajitambue.Tusaidieni tujijue na tujue adui yetu kwa taarifa za uhakika. Na kama mkiambatanisha taarifa hizi eg mkaweka vedio clips,,,basi kocha anaweza penyezewa akaangalia na kusaidia kubadili mbinu za mchezo.Tuangalie taarifa zetu kwa jicho la kusapoti team zetu na watu wetu

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV