June 4, 2016

MALIMA
Saa 24 baada ya Mwenyeki wa Yanga, Yusuf Manji kuwafuta uanachama wanachama tisa wa klabu hiyo, beki wa zamani wa timu hiyo, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ ameupokea kwa mikono miwili uamuzi huo huku akikiri kuwa kitendo alichokifanya ni kosa.

Malima na wenzake nane, walienda kuchukua fomu za kuwania uongozi ndani ya Yanga katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kuonekana kwenda kinyume na taratibu za klabu hiyo.

Wanachama wengine waliofutwa uanachama na Manji kwa kosa hilo ni Aaron Nyanda, Titus Kibula, Pascal Raiza, Amir Mataka, Said Omary, Ally Chokoma na Amiri Msumi ambaye ni mwenyekiti wa matawi ya timu hiyo.

Wote hao kwa kitendo walichofanya, wanatuhumiwa kushiriki katika mipango ya kuuhujumu uongozi uliopo madarakani.

Jembe Ulaya alisema hapingi uamuzi wa kusimamishwa kwake na uongozi wa klabu hiyo baada ya kugundua kosa alilolifanya ila amesisitiza kuendelea kuisapoti Yanga.

 “Sikujua kuwa TFF hawapaswi kuendesha uchaguzi wa Yanga ila ukimya wa viongozi wa Yanga ndiyo ukanifanya niende TFF nikiamini wapo sahihi, hata hivyo nitaendelea kuiunga mkono Yanga,” alisema Jembe Ulaya.

Kwa upande wake, Msumi amesema: “Nimesikia kuhusu kufutwa kwangu uanachama lakini mtu mmoja hana mamlaka ya kufuta watu uanachama kwa mujibu wa Katiba ya Yanga.

“Kama mtu ametenda kosa, anapewa barua na kuitwa kwenye kamati kwa ajili ya kujielezea, ikishindikana anatakiwa apelekwe kwenye mkutano mkuu akajadiliwe kwani wenye kauli ya mwisho ni wanachama.

“Pia zile sauti zinazolalamikiwa kweli ni zangu lakini hakuna sehemu inayotaja mambo ya rushwa, naomba ieleweke hivyo. Ila Yanga ni kitu kimoja haihitaji sababu za kufarakana.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic