June 4, 2016


Straika Mbwana Samatta wa KRC Genk amesema Yanga kama ikijipanga inaweza kuifunga TP Mazembe katika mechi yao ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga itacheza na TP Mazembe ya DR Congo kati ya Juni 28 na 29, mwaka huu jijini Dar es Salaam mchezo wa kwanza wa Kundi A la Kombe la Shirikisho. 

Samatta aliyewahi kuichezea TP Mazembe akitokea Simba, ameliambia Championi Jumamosi kuwa, Yanga inaweza  kuiondoa TP Mazembe katika michuano hiyo kama ikijipanga ipasavyo.

Alisema anaamini hilo linawezekana kwani kikosi cha Yanga hivi sasa kipo vizuri ukilinganisha na misimu mingine iliyopita.

 “Hali hiyo ndiyo inayonifanya niamini kuwa Yanga inaweza kuifunga TP Mazembe, kwani nimekuwa nikiifuatilia sana na kuona jinsi wachezaji wake wanavyopambana uwanjani.

“Hata hivyo Yanga wanatakiwa kujipanga na kukiandaa kikosi chao kwa ajili ya michuano hiyo, kama kuna upungufu ambao waliuona hapo awali basi muda huu ndiyo wa kuufanyia kazi kabla ya kuanza kwa hatua hiyo makundi.

“TP Mazembe ni timu nzuri na yenye mafanikio Afrika, lakini katika soka lolote linaweza kutoka ndiyo maana nimesema Yanga inaweza kuifunga timu hiyo kama ikijiandaa vizuri,” alisema Samatta ambaye leo ataichezea Taifa Stars dhidi ya Misri.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic