June 28, 2016


Kocha Antonio Conte ameiwezesha Italia kuivua ubingwa wa Euro Hispania. Kama hiyo haitoshi, ameiwezesha Italia kutinga robo fainali ya michuano hiyo inayoendelea nchini Ufaransa.

Lakini gumzo zaidi la Conte ni vituko vyake anapokuwa kwenye benchi wakati timu yake inashambuliwa au kushambulia.

Lakini hatari zaidi ni pale timu yake inapopata bao au kuibuka na ushindi. Midadi yake, vituko vyake ni hatari. Kumbuka huyu ndiye kocha mpya wa Chelsea ya England.

Ligi Kuu England wajiandae kukutana na vituko vyake na itakuwa ni sehemu ya burudani ya ligi hiyo inayotarajia kurejea katika kiwango chake cha juu.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV