June 12, 2016Kamati ya Usajili ya Simba na ile ya ufundi, zimeendelea kukutana kujadili masuala ya usajili.

Kamati hizo mbili nyeti za usajili za Simba, zimeendelea kukutana na kujadili masuala yanayohusiana na usajili kwa kuwa kuna majina mengi ambayo wanapaswa kupata uhakika.

Taarifa za awali zinaeleza kikao cha kwanza kilifanyika juzi, lakini imeelezwa hata leo kulikuwa na kikao kingine tena kuhusiana na masuala hayo ya usajili.

Inaonekana Simba wameendelea na mfumo wao ule wa kufanya mambo kwa siri kama ilivyokuwa msimu uliopita ambao hata hivyo hawakufanikiwa sana.

Simba iliishia katika nafasi ya tatu katika ligi kuu na kuwaacha watani wao Yanga wakiendelea kutamba zaidi kwa kubeba ubingwa na Azam FC nafasi ya pili.

Pia ilitolewa kwenye nusu fainali ya Kombe la FA na kibonde Coastal Union ambao waliteremka daraja.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV