June 12, 2016


Baada ya kukimbia ushindani Yanga, Paul Nonga anarejea Mwadui FC.

Taarifa za ndani kutoka Yanga zinaeleza, tayari wamekubali kumuachia Nonga arejee Mwadui FC ambayo ilimuuza Yanga.
Hata hivyo kumekuwa hakuna uhakika kama Nonga atauzwa moja kwa moja tena au atapelekwa kwa mkopo.

Mshambuliaji huyo ameamua kuandika barua kuomba kuondoka baada ya kuona hawezi kuendelea kushindana na Donald Ngoma na Amissi Tambwe na kupata namba ya kucheza.


Lakini awali hakukuwa na uhakika kuhusiana na ruhusa yake kama kweli imepita au la.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV