June 12, 2016


Beki mpya wa Yanga, Hassan Kessy amekuwa kivutio mitandaoni kutokana na picha zake mbalimbali akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kwenda Antalya nchini Uturuki.

Beki huyo wa zamani wa Simba amekuwa akipiga picha nyingi na kuzitupia mtandaoni akionyesha furaha yake ya kwenda Uturuki kuweka kambi.

Katika picha hizo, Kessy ameonekana ni mtu mwenye furaha kuu ambaye yuko tayari sasa kuitumikia Yanga.


Kikosi cha Yanga  kimeondoka leo alfajiri kipo mjini Antalya nchini Uturuki ambako wameweka kambi kujiandaa na mechi yao dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali.


2 COMMENTS:

  1. Kupanda ndege wewe?Angebaki Chura Sc kamwe hasingekwenda Ulaya hata kwa shoka!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaani ndege imekuwa issue! Wabongo bwana! Hv hamjui kama mnamdhalilisha kwa kumuona mshamba wa ndege! Angekuwa anjitambua asingechekelea sifa za Kijinga hizo!

      Delete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV