June 29, 2016

KICHUYA (MBELE) AKIPAMBANA NA MOHAMED ZIMBWE WA SIMBA.

Kiungo mshambuliaji wa Mtibwa Sugar anayetarajia kutua Simba, Shiza Kichuya yupo katika mazoezi makali ya saa nne kila siku ili kujiimarisha kuhakikisha anatoa ushindani wa kutosha msimu ujao.

Kichuya ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa mbioni kusajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili kwa dau la Sh milioni 20, ili kuisaidia timu hiyo msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Kichuya amefunguka kuwa, tangu atoke Taifa Stars amekuwa mtu wa kupiga tizi kwa saa nne kwa siku katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Morogoro, mkoani Morogoro ili kuleta ushindani katika timu yake mpya.

“Nimeanza kufanya mazoezi binafsi kwa saa nne kwa siku tangu nilivyotoka katika kikosi cha timu ya taifa lengo likiwa ni kujiimarisha na kuhakikisha naleta ushindani msimu ujao kama ilivyokuwa msimu uliopita nikiwa Mtibwa.


“Haijalishi kama nitakuwa Simba ama nitabaki hapahapa (Mtibwa) lengo langu ni kuendelea kuwa fiti zaidi na kuleta ushindani na hata nikiwa Simba ninachohitaji ni kupata namba na sehemu yenye ushindani ndiyo ninayoipenda zaidi kwani inanisaidia katika kujiweka fiti,” alisema Kichuya.]

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV