June 29, 2016Wakiwa kwenye maandalizi ya mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe, beki mpya wa Yanga, Hassan Kessy amewekwa kitimoto na kocha wake Mholanzi, Hans van Der Pluijm kwa siku mbili.

Beki huyo, hivi sasa yupo kwenye mgogoro na uongozi wa Simba ukidai mchezaji huyo ni mali yao bado huku mwenyewe akisema mkataba wake umemalizika tangu Juni 15, mwaka huu.

Sakata hilo, lilianza wakati timu hiyo ilipopanga kumtumia nyota huyo kwenye mechi na MO Bejaia ya Algeria wakati beki wao Juma Abdul akiwa nje ya uwanja akiuguza majeraha ya enka.

Kessy alisema kikao cha kwanza walikifanya wakiwa kambini Uturuki, akiwa chumbani kocha alimfuata na kumuhoji akitaka kujua ukweli wa mkataba wake siku moja kabla ya mechi na MO Bejaia.

Kessy alisema, katika kikao hicho, alijaribu kumfafanulia ukweli wa mkataba wake uliomalizika tangu Juni 15, mwaka huu, hivyo anashangaa kuona viongozi wa Simba wakiendelea kumng'ang’ania kuwa ni mali yao huku wakigoma kutoa barua kumruhusu kuondoka.

Aliongeza kuwa, kikao kingine walikifanya na kocha huyo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kabla ya mazoezi ya asubuhi siku moja kabla ya mechi na TP Mazembe, ambapo anasema alitumia dakika tano kumwelezea kwa undani na akamuelewa, hivyo akashangaa kuona Simba wakimuwekea ngumu.

"Leo (jana) meneja wangu na Chama cha Wachezaji Tanzania (Sputanza) wakiwa na mkataba wangu wataelekea TFF kwa ajili ya kwenda kuishtaki Simba wanaodai kuwa mimi ni mali yao.

"Hilo suala ni ndogo sana, lakini wenyewe wanataka kulifanya kuona kubwa, ninaamini hilo litamalizika hivi karibuni baada ya meneja wangu na Sputanza kulifikisha TFF ili ukweli upatikane.


"Nakosa furaha kwenye timu yangu mpya ya Yanga na mimi ninataka kucheza na kitu kikubwa kinachonichanganya, kocha mwenyewe anaonekana kutaka kunitumia, lakini inashindikana kutokana na hali hiyo, nimefanya naye kikao mara mbili akihoji mkataba wangu akitaka kujua ukweli,"alisema Kessy.

SOURCE: CHAMPIONI

.

4 COMMENTS:

 1. Hivi hawa wanaojiita SPUTANZA mbona huwa wanasikika kwenye kesi za usajili zunazoihusu Yanga pekee?Kimsingi hakuna aliyepinga usajili wa Kessy kwenda yanga,haraka ya nini asubiri buda wa taratibu za uhamisho uliowekwa na TFF ufike ataruhusiwa kwenda kuichezea timu anayiipenda ambayo alikuwa anaibeba kila ikutanapo na simba kwa kujisababishia kadi za kijinga na kutoa pasi za Mwisho kwa Ngoma ili akafunge.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Unaonekana ni limbukeni na hata mpira haujui, kesi ya singano ilihusisha Yanga!? Simba imekuwa inakwaruzana na SPUTANZA kwa sababu ya tabia yao ya kuforge mikataba!!

   Delete
 2. Kessy ni mali ya Yanga, lakini muda wa usajili na kumalizika vipingamizi ni mwezi wa nane. Kwa hiyo sio Simba wanaomzuia, bali taratibu za TFF

  ReplyDelete
  Replies
  1. ipo aja ya kuwa na semina zina zouhusiana na mawsala ya mikataba kwa wachezaji hapa napo kess hanaonekana hajui sababu inayo mfanya hashindwe kucheza anatupa lawama tu kwa simba .wacheza viongozi na hata hao sputanza hawa jui nin kinaitajika

   Delete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV