June 25, 2016


Kiungo mpya wa Simba, Mohammed Ibrahim ameendelea kujifua zaidi kabla ya Simba haijaanza rasmi maandalizi ya msimu mpya.

Taariafa zinaeleza, Simba inatarajia kuanza mazoezi rasmi Juni 27 lakini Ibrahim aliyejiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar, hajataka kusubiri.


Kwanza alianza na mazoezi ya gym kwa kipindi kadhaa ikiwa ni siku chache baada ya kujiunga na Simba kwa miaka miwili.

Lakini sasa ameonekana katika Uwanja wa Garden uliopo Vijana-Kinondoni jijini Dar es Salaam akijiweka vizuri.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV