June 25, 2016
Fowadi wa Simba, Daniel 'Danny Lyanga akimiliki mpira katika mazoezi yanayowakutanisha wachezaji mbalimbali wa timu za madaraja tofauti zikiwemo za Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Garden uliopo Vijana-Kinondoni jijini Dar es Saalaam.


Lyanga na Said Ndemla ambao ni wachezaji wa Simba, wamekuwa wakiendelea kujiweka fiti kiana kabla ya timu hiyo kuanza mazoezi rasmi kujiandaa na msimu ujao chini ya Kocha Mkuu, Joseph Omog.

Pamoja na Lyanga na Ndemla, nyota wengine wa Simba na timu nyingine za Ligi Kuu Bara wamekuwa wakijitokeza kwenye Uwanja wa Garden kujifua.

Wengine ambao walionekana kwenye Uwanja wa Garden ni pamoja na William Lucian 'Gallas' na Aziz Sibo (Ndanda), Rashid Mandawa (Mwadui), Peter Manyika, Mohamed Ibrahim 'Rasta' (Simba), Hussein Sharrif 'Casillas' na Seleman Kibuta (Mtibwa Sugar).

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV