June 6, 2016PASUWA


Mafanikio ya wachezaji wa Zimbambwe akiwemo mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma, yanaonekana kuwavuta viongozi wa Simba ambao jana walikuwa jijini Harare nchini Zimbabwe.

Zacharia Hans Poppe ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, pamoja na wajumbe Said Tully na Collins Frisch, jana walikuwa uwanjani wakati Zambia ikiitwanga Malawi kwa mabao 3-0, jana. Lengo ni kumalizana na kocha wa timu ya taifa ya Zimbabwe.

Simba walikuwa wanasubiri kocha wa Kalisto Pasuwa amalize mechi ili wafanye naye mazungumzo.

“Kweli tuko uwanjani hapa, hivyo siwezi kuzungumza lolote,” alisema Hans Poppe.

Lakini taarifa za uhakika zilieleza baada ya mechi, viongozi hao wa Simba wakiongozwa na Hans Poppe walifanikiwa kufanya mazungumzo na kocha huyo na amekubali kutua Simba.

“Pasuwa amekubali kutua Simba, ni mambo machache yamebaki na anahitaji kupata maslahi yake anayodai Zimbabwe,” kilieleza chanzo.

“Juhudi bado zinafanyika, yeye anaona mazingira ya mkataba wa Simba anakubaliana nao. Kikubwa zaidi sasa ni suala la yeye kumalizana na shirikisho la Zambia.”

Pasuwa ndiyo chaguo la kwanza la Simba, ikishindikana kabisa, Simba imepanga kumuajiri kocha raia wa Senegal na Joseph Omog kocha wa zamani wa Azam FC raia wa Cameroon, yeye anaonekana kuwa chaguo la tatu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV