June 6, 2016


NYIRENDA
Uongozi wa Simba unaonyesha umepania kuimarisha nguvu ya kikosi chake kwa juhudi kubwa, sasa imepanga kumsajili beki wa kati wa timu ya taifa ya Malawi ambaye ni Harry Nyirenda.

Nyirenda anayekipiga Black Leopards ya Afrika Kusini, jana aliingoza Malawi ugenini kuivaa Zimbabwe na wenyeji wakashinda kwa mabao 2-0.

Zacharia Hans Poppe ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, pamoja na wajumbe Said Tully na Collins Frisch, jana walikuwa uwanjani wakati Zimbabwe ikiimaliza Malawi kwa mabao 2-0 na Nyirenda akionyesha soka safi.

“Ndiyo Nyirenda ni sehemu ya wachezaji ambao Simba inawataka na mazungumzo bado yanaendelea,” kilieleza chanzo.


Moja ya kazi kubwa kwa Hans Poppe na timu yake iliyosafiri kwenda Harare, Zimbabwe ilikuwa ni kufanya mazungumzo na beki huyo kwa ajili ya kuimarisha ukuta wa Simba.

Kamati ya usajili ya Simba pamoja na uongozi wa klabu hiyo, umekuwa ukihaha kuimarisha kikosi chao ambacho msimu uliopita kiliambulia nafasi ya tatu.


Hali hiyo imeufanya uongozi wa Simba kuhakikisha unapata wachezaji bora huku ukipanga kuwatema wengi ambao wakionekana ‘kuzingua’ mwishoni mwa msimu uliopita.a

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV