June 28, 2016


Mashabiki wa Yanga walianza kufika Uwanja wa Taifa kuanzia saa 12 asubuhi ili kuhakikisha wanapata nafasi ya kuishuhudia timu yao ikipambana na TP Mazembe.

Mashabiki hao,  walionekana kila mmoja amepania kupata nafasi na wengi walikuwa na hofu ya kutopata kwa kuwa uamuzi wa uongozi wa Yanga kuondoa kabisa kiingilio, walijua utachangia wingi wa watu.

Yanga inaivaa TP Mazembe katika mechi ya Kombe la Shirikisho ambayo kama watashinda, watakuwa wamefufua matumaini upya baada ya kuwa wameanza michuano hiyo hatua ya makundi kwa kupoteza dhidi ya Mo Bejaia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV