June 10, 2016Kiungo mpya wa Yanga, Juma Mahadhi ameanza kuonyesha  cheche zake baada ya kufanikiwa kufunga mabao mawili katika mazoezi  ya timu hiyo yaliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar huku akifanikiwa kutengeneza penalti mbili.

Mahadhi ambaye amejiunga na Yanga akitokea Coastal Union ya Tanga iliyoshuka daraja msimu ulioisha, alikuwa akishangiliwa na mashabiki karibu kwa kila alichokuwa akifanya uwanjani.

Katika mazoezi hayo kiungo huyo akionyesha uwezo mkubwa  ambao alikuwa kivutio kwa kocha wa makipa wa timu hiyo, Juma Pondamali na Kocha Mkuu Mholanzi, Hans van Der Pluijm.

Kiungo huyo alifunga bao lake la kwanza baada ya kupata pasi kutoka kwa Donald Ngoma ambapo aliwazidi kasi mabeki, Juma Makapu na Haji Mwinyi kisha akamfunga Kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ kirahisi.

Mara baada ya bao hilo, Mahadhi na wenzake walikwenda mapumziko na aliporudi alipokea pasi toka kwa Hassan Kessy na kufunga kwa ufundi wa hali ya juu kwa shuti kali.

Licha ya mabao hayo, Mahadhi pia alikuwa mwiba kwa beki wa kushoto wa timu hiyo,  Mwinyi kutokana na kumpita kila wakati kabla ya kumchezea rafu ndani ya eneo la 18 na kusababisha penalti iliyotokana na beki huyo kuzidiwa ujanja, penalti ambayo ilifungwa na  Mzimbabwe, Donald Ngoma.

Katika kuonyesha amekuja kikazi ndani ya kikosi hicho, Mahadhi  alifanikiwa kusabisha penalti ya pili ambayo pia ilifungwa na Ngoma baada ya kumzidi kasi beki wa kati wa timu hiyo, Pato Ngonyani na kumchezea rafu ya nyuma kama ilivyokuwa kwa Mwinyi, kitendo kilichosababisha Pluijm ‘kumwakia’ Pato kutokana na uzembe huo huku akimpongeza kiungo huyo kwa uwezo mkubwa aliounyesha kwenye mazoezi hayo.

   

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV