June 9, 2016


Mashabiki Simba wameanza kuingia hofu kwamba uongozi wao haufanyi lolote kuhusiana na usajili.

Hofu hiyo inaingia baada ya kuona Yanga ikiendelea kusajili mfululizo lakini wao wakiwa hawajafanya jambo.

Baadhi ya waliotuma maoni katika email ya mtandao wa SALEHJEMBE wamekuwa wakilalama kwamba suala la usajili kwao linaonekana kwenda taratibu.

Wengine waliutaka uongozi wa Simba kuinua macho haraka na kuangalia uwezekano wa kufanya usajili sahihi.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema kila kitu kinaendelea kwa mpangilio.

“Kila kitu kinakwenda vizuri, hatuna sababu ya kuwa na haraka. Yanga wanakwenda na mipango yao na sisi tuna yetu.

“Wao wanaanza maandalizi sasa, sisi muda bado. Lakini si kweli tumekaa tu na si kila tunachofanya kitangazwe,” alisema.

Tayari Hans Poppe alishasafiri hadi Zimbabwe ingawa alisema ni masuala yake binafsi, lakini alishughulikia masuala ya usajili pia.


1 COMMENTS:

  1. Bdjobs today all newspaper jobs in one click

    Today match sports live score

    HSC resul ALL Result 2016

    DU admission DU admission test result 2016-17

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV