June 10, 2016


Polisi wa jiji la French Marseille nchini Ufaransa wamelazimika kufanya kazi ya ziada kuwathibiti mashabiki wa England ambao walilewa na kuanza kufanya vurugu.

Mashabiki hao ambao wako Ufaransa kwa ajili ya michuano ya Euro 2016 walikuwa wakifanya vurugu huku wakiimba nyimbo za kuwasaka magaidi ya ISIS.

Walikuwa wakiuliza walipo ili wapambane nao huku wakisisitiza kama wao ni wanaume wa shoka basi wajitokeze.

Jiji la Marseille linaelezwa kuwa na Waislamu wengi ambao wanachukua robo tatu ya wakazi wake na hii inatokana na kuwa na wahamiaji wengi zaidi kutoka katika nchi za Kaskazini mwa Afrika ambazo asili yao ni Waarabu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV