June 1, 2016
Mbeya City  imepaga kujiandaa kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara kwa kucheza mechi za kirafiki nchini Malawi.

Kikosi cha Mbeya City chini ya Kocha Kinnah Phiri kinatarajia kucheza michezo mitatu nchini Malawi ambako ni kwao Phiri.

Mechi ya kwanza ya kikosi cha City itakuwa ni Juni 18 kwenye Uwanja wa Kamuzu mjini na watakutana na moja ya timu kongwe  za Malawi, Big Bullets.

City itarejea dimbani Juni 21 kuwavaa Civo United kabla ya kumaliza mechi ya tatu ambayo itatajwa hapo baadaye.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV