June 1, 2016Beki mpya wa Yanga, Hassan Kessy amesema anajua ushindani mkali ulio katika kikosi cha Yanga kuliko Simba.

Kessy amejiunga na Yanga akitokea Simba ambako mkataba wake umeshamalizika.

Akizungumza mjini Morogoro, Kessy amesema ushindani ni mkubwa ndiyo maana ameamua kuendelea na mazoezi hata katika kipindi hiki cha mapumziko.

Amekuwa akifanya mazoezi gym na wakati mwingine uwanjani ili kuhakikisha anakuwa vizuri.

“Lazima kufanya mazoezi ili niingie katika kikosi nikiwa tayari, ushindani Yanga ni mkubwa kama unavyojua.


“Lakini ninafurahia kwa kuwa ushindani humfanya mtu awe imara, hivyo niko tayari kupambana na kuisaidia timu yangu mpya,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV