June 7, 2016


Kiungo Mholanzi Memphis Depay hana uhakika kama ataendelea kubaki katika kikosi cha Manchester United chini ya Kocha mpya, Jose Mourinho.

Depay ameanza kuhamisha vita vyake kurudisha kwao nchini Uholanzi akianza na magari yake ya kifahari.


Gari lake la kifahari aina ya Mercedes G Wagon lenye thamani ya pauni 100,000 pamoja na pikipiki aina ya Scorpion yenye thamani ya pauni 13,500 pia zimepelekwa kwao Uholanzi.


Tayari kuna taarifa Mholanzi huyo mwenye miaka 22, alianza kusafirisha gari lake la kifahari zaidi aina ya Rolls Royce Wraith lenye thamani ya pauni 250,000 kulirejesha kwao Uholanzi. Hata hivyo, bado Mourinho hajaanza usajili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV