June 23, 2016Nyota Lionel Messi amekuwa mfungaji mwenye mabao mengi zaidi kuliko wengine wote kwa kipindi chote katika kikosi cha Argentina.

Messi alifikisha mabao 55 wakati alipoingiza Argentina kuitwanga Marekani kwa mabao 4-0 katika mechi ya nusu fainali ya Copa America.


Kwa rekodi hiyo, mshambuliaji huyo nyota wa Barcelona ameungana na washambuliaji nyota wengine walio na rekodi za juu kama Robin van Persie na Uholanzi, Zlatan Ibrahimovich na Sweden, Thierry Henry na Ufaransa au Pele na Brazil.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV