June 23, 2016

 
Staa LeBron James hana mpango hata kidogo wa kuondoka Cleveland Cavaliers.

Cavaliers inamlipa jumla ya dola million 23 kwa mwaka. Naye amesema baada ya kuiwezesha kubeba ubingwa, angependelea kuendelea kubaki.

Mchezaji kikapu huyo maarufu kama King James, ameiwezesha Cavaliers kubeba ubingwa wa NBA tena baada ya kuwa imefanya hivyo mwaka 1964.

Mashabiki walijitokeza kwa wingi kuipokea timu hiyo na kumpongeza yeye katokana na kazi nzuri aliyoifanya ya kuiangusha Golden State iliyokuwa inapewa nafasi kubwa ya kubeba ubingwa wa NBA.
 
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV