June 6, 2016

SAMATTA
Kocha Mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars, Charles Mkwasa ameeleza kuwa penalti aliyokosa nahodha wa timu hiyo, Mbwana Samatta, wakati wanapambana na Misri, ilichangia kuwavuruga katika mchezo huo waliofungwa mabao 2-0.

Matokeo hayo ya mchezo huo uliopigwa juzi Uwanja wa Taifa, Dar yaliiondoa Stars katika kuwania kufuzu michuano ya Mataifa Afrika (Afcon), mwakani huko Gabon ambapo kwa ushindi huo Misri imefikisha pointi 10, ambazo hazifikiwi na Stars wala Nigeria zilizo kwenye kundi lake.

MKWASA

Hata hivyo, Mkwasa alifafanua kuwa kama Samatta angefanikiwa kufunga penalti hiyo na kusawazisha matokeo kuwa 1-1, hiyo ingeongeza nguvu kwa Stars na kuwavuruga Misri.

"Tumepata penalti, lakini bahati mbaya tumekosa. Kama Samatta angepata ile penalti ingetusaidia maana Wamisri wangevurugika na sisi tungeibua nguvu mpya kabisa, lakini haikuwa hivyo na huwezi kulaumu maana penalti inajulikana.

"Soka ni mchezo wa saikolojia pia, unajua baada ya kukosa ile penalti, Wamisri walipata nguvu na sisi tukawa kama tumenyong'onyea na mwisho ile ari ikapungua na kuwapa mwanya wapinzani wetu.


"Siwezi kukataa Wamisri ni wazuri na ni timu ngumu lakini ukiangalia mabao yao yalikuwa mepesi, si ya kusema wamepambana sana kuyapata, ukitazama bao la pili ni kosa la ulinzi tu ndiyo limetugharimu," alisema Mkwasa.

1 COMMENTS:

  1. Ile penati inaitwa "PENATI YA MWENDO KASI"!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic