June 6, 2016Beki mkimya wa Simba, Mohammed Hussein ameamua kuachana na jina lake la utani la Tshabalala.

Hussein ambaye ni beki wa kushoto anayeonekana kuja kwa kasi zaidi katika kipindi hiki, ameamua kuachana na jina hilo ambalo kiasili ni mali ya kiungo wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Shiphiwe Tshabalala.

“Sasa nitatumia Zimbwe, hili ni jina la babu yangu mzaa mama,” anasema Hussein.

SALEHJEMBE: Lina uhusiano na wale kina Zimbwe waliowahi kucheza Yanga, mfano Said Zimbwe?

HUSSEIN: Kabisa.

SALEHJEMBE: Kivipi, fafanua kidogo…


HUSSEIN: Wale ni wajomba zangu, wamechangia baba na mama yangu mzazi. Vizuri sasa nikijulikana kwa jina hilo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV