June 22, 2016


Maharage Ally Chande ni Mtanzania, amefanikiwa kuweka rekodi kwenye Kampuni ya MultiChoice Tanzania, baada ya kuteuliwa kuwa mtendaji mpya wa kampuni hiyo.

Rekodi aliyoiweka Chande ni kwamba anakuwa Mtanzania wa kwanza kushika wadhifa huo wa juu ndani ya MultiChoice Tanzania, ambapo kabla ya hapo aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi katika Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi.

Mwenyekitiwa MultiChoice Tanzania, Ami Mpungwe, amesema; “MultiChoice Tanzania inaona fahari kuhusu uteuzi huu, hakuna shaka kwamba Chande ni miongoni mwa Watanzania watendaji bora kabisa.


“Sifa zake kama mtaalamu wa huduma za kibenki na kifedha pamoja na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ni ujuzi tunaouhitaji katika biashara yetu ili kuipeleka biashara ya Tanzania katika viwango vipya vya hali ya juu, tunamtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya na bila shaka atawahudumia wateja wetu wa DSTV kwa nguvu na juhudi mpya.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV