June 22, 2016
Beki Juma Abdul ameanza mazoezi taratibu jijini Dar es Salaam ikiwa ni baada ya kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki moja.

Yanga ipo mjini Antalya, Uturuki ikijiandaa dhidi ya TP Mazembe, mechi itakayopigwa Jumanne ijayo jijini Dar.

Juma amekuwa majeruhi na alilazimika kubaki nchini wakati Yanga ikisafiri kwenda Uturuki kuweka kambi na baadaye kwenda Algeria kuivaa Mo Bejaia.

Yanga imepoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Mo Bejaia katika mechi yake ya kwanza ya Kombe la Shirikisho hatua ya makundi.

Beki huyo wa kulia maarufu kwa ukunjaji krosi zenye macho, ameanza mazoezi ya taratibu na ataendelea taratibu kutokana na maelekezo ya dakitari.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV