June 17, 2016

 Mzambia Obey Chirwa rasmi amesaini kuichezea Yanga, ameingia nayo mkataba wa miaka miwili na kufunga idadi ya wachezaji saba wa kulipwa.

Chirwa anayetokea FC Platinums ya Zimbabwe amesaini mkataba huo leo mbele ya Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deudetis.

Taarifa zinaeleza kuwa Yanga imemwaga kitita cha dola 100,000 (zaidi ya Sh milioni 200) ili kumalizana na timu yake na mshambuliaji huyo.

Kesho alfajiri, anatarajia kuondoka nchini kwenda Algeria kuungana na kikosi cha Yanga ambacho kinacheza dhidi ya Mo Bejaia.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV