June 23, 2016


Mshambuliaji mpya wa Yanga, Obey Chirwa ameanza mazoezi na kikosi cha Yanga kilicho kambini nchini Uturuki.

Yanga inanolewa na Mholanzi, Hans van der Pluijm na Chirwa atalazimika kuanza kuzoea taratibu mbinu za kocha wake huyo mpya ambaye ameifikisha Yanga hatua hiyo.

Chirwa raia wa Zambia aliyejiunga na Yanga akitokea FC Platnums ya Zimbabwe anatarajia kuongeza nguvu safu ya ushambuliaji ya Jangwani katika mechi iijayo ya Kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo.

Picha zinaonyesha Chirwa mazoezini na wenzake nchini Uturuki na anaonekana tayari ameanza kuizoea hali ya ndani ya kikosi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV