Kocha Hans van der Pluijm ameanza kukinoa kikosi chake kwa masomo maalum kuhakikisha wanajifunza mengi kuhusiana na mifumo.
Yanga ipo kambini nchini Uturuki kwenye mji wa kitalii wa Antalya ambao uko ufukweni kabisa.
Pluijm raia wa Uholanzi amekuwa akiwafua vijana wake usiku kwa ajili ya kuangalia muda ambao wataanza kucheza mechi yao ya kwanza ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Mo Bejaia ya nchini Algeria.
Lakini sasa wamekuwa wakitumia muda wao kadhaa kujifunza kutumia 'screen' maalum pamoja na mambo kadhaa yanayohifadhiwa kwenye kompyuta hasa yanayohusiana na mifumo.
Somo hilo limekuwa likiendelea mara kadhaa, ikiwa ni sehemu ya Pluijm kuhakikisha kambi hiyo ya Uturuki inaza matunda.
0 COMMENTS:
Post a Comment