June 29, 2016


Rais wa Argentina, Mauricio Macri amesema atafanya juu chini kumshawishi atakapokutana na Lionel Messi abadili msimamo wake wa kustaafu kuichezea timu ya taifa.

 Macri amesema anatarajia kukutana na Messi wiki ijayo na atazungumza naye kuhusiana na hilo. Wakati yeye anasema hivyo, jiji la Buenos Aires wamezindua sanamu lake.


Sanamu hilo tayari limekuwa kivutio kikubwa miongoni mwa mashabiki wa soka.

Messi alitangaza kustaafu kuichezea Argentina baada ya mechi ya fainali ya Copa America na kupoteza kwa penalti 4-2 dhidi ya Chile.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV