June 29, 2016


Kuna taarifa zinaelezwa kwamba kuna uharibifu mkubwa umefanyika ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya mechi ya jana.

Lakini habari nyingine za uchunguzi zinaeleza, taarifa hizo zimekuwa zikitengenezwa kwa ajili ya kuhakikisha Yanga inatoboka mifuko ili kulipa gharama.

Mmoja wa watu waliokuwa wakisimamia ulinzi kwenye Uwanja wa Taifa, jana wakati Yanga ilipoivaa TP Mazembe na mashabiki kuingia bure amesema, hadi wanaondoka hakukuwa na uharibifu zaidi ya sehemu ya geti ambayo ilivunjwa na mashabiki.

“Sehemu ya uzio ambao mashabiki walivunja ni kweli. Lakini kusema kuna uharibifu mkubwa ni hadithi tu na huenda kuna watu wana hasira na Yanga.

“Unajua kuna ambao wamekosa mapato baada ya Yanga kuamua mashabiki kuingia bure.

“Sasa wanaweza wakawa wanafanya figisu nao kuikomoa Yanga kwa kuwa wanaona kama imewakomoa kwa kuamua mechi iwe bure.

“Lakini ukweli hakuna uharibifu wowote mkubwa kama inavyoelezwa,” kilieleza chanzo.

Lakini Msemaji wa TFF, Alfred Lucas Mapunda, yeye amesisitiza kuna uharibifu.

“Tulikaa pale hadi saa tatu usiku, kuna uharibifu umetokea sehemu mbalimbali mfano uzio umevunjwa, kuna mabomba ya gesi yameng’olewa.


“Tumeacha wafanye tathmini halafu tutaangalia kama ni ghara ambazo wanatakiwa Ynga kuingia, basi watapewa taarifa,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic