June 29, 2016



Na Saleh Ally
Sare ya bila kufunga kati ya Medeama iliyokuwa nyumbani dhidi ya Mo Bejaia jijini Accra, leo, imezidi kuiweka Yanga katika wakati mgumu zaidi.

Sare hiyo ya leo, imeipa Mo Bejaia pointi moja, hivyo kufikisha pointi nne na Medeama ikiandikisha pointi ya kwanza.

Kupata pointi kwa Medeama ya Ghana, kunaifanya Yanga kuendelea kubaki mkiani lakini kuwa timu pekee ambayo haina pointi hata moja.

Ugumu unazidi kwa Yanga kwa kuwa inatakiwa kushinda mechi zake mbili zijazo ili kuanza kupanda tena.

TP Mazembe inaongoza kundi A kwa kuwa na pointi 6 baada ya ushindi dhidi ya Medeama kwa mabao 3-1 kabla ya kuichapa Yanga kwa bao 1-0.

Mo Bejaia inafuatia ikiwa na pointi nne baada ya kuifunga Yanga bao 1-0 na baadaye sare ya leo. Sasa wana pointi nne katika nafasi ya pili.

Medeama waliopoteza kwa mabao 3-1 Lubumbashi na sare ya leo, maana yake wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi moja na huenda wakaamsha matumaini zaidi kama watafanya vizuri dhidi ya Yanga ambayo ni mechi ijayo.

Lakini Yanga ikishinda dhidi ya Medeama, itakuwa imeamsha matumaini tena kwa kuwa itaishusha Medeama mkiani na kuanza kupambana na Bejaia ili kupata nafasi.

TP Mazembe inaonekana imeishaichukua moja ya nafasi mbili za kufuzu kwenda hatua ya nusu fainali.


Katika soka, lolote linawezekana lakini Yanga inalazimika kufanya kazi ya ziada kugeuza asilimia za kusonga mbele ilizonazo kwa sasa kwa kuwa kama ni nyingi, basi ni 15 tu.

1 COMMENTS:

  1. Makofia keshasema watafungwa mechi zote,hata ya nyumbani.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic