June 29, 2016


Nahodha wa Ureno, Cristiano Ronaldo ameonyesha mbwembwe zake za ‘msuli’ ikiwa ni ishara ya kuonyesha kuwa yuko tayari.

Ronaldo anaonyesha yuko tayari kwa ajili ya mechi ya robo fainali ya michuano ya Euro dhidi ya Polandi.

Mechi itapigwa keshokutwa Alhamisi na Ureno wana matumaini kwamba kikosi chao kimekaa vizuri sasa kuendelea kupambana.


Michuano ya Euro inaendelea nchini Ufaransa na Ureno imekuwa ikisonga mbele "kimkandamkanda", jambo ambalo linafanya watathmini wasiipe nafasi kubwa hata ya kufika fainali.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV