June 30, 2016

CHANONGO (KULIA) AKIWA NA MAGURI AMBAYE BAADA YA KUMALIZA MKATABA NA STAND, AMETIMKIA UARABUNI


Uongozi wa klabu ya Stand United, umekanusha kumuacha Haruna Chanongo na kusema tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea.

Katibu Mkuu wa Stand United, Dk Jonas Tiboroha amesema kuna kundi ambalo linawavuruga kwa kutoa habari zisizo sahihi kwa kushirikiana na baadhi ya vyombo vya habari.

“Chanongo amesaini mkataba wa miaka miwili, kuna watu wanafanya makusudi kutuvuruga huku wakijua si sahihi.


“Niwaombe wanahabari kwamba watu wanaoweza kuwapa taarifa sahihi ni Mwenyekiti Amani Vicent, mimi au Msemaji wa klabu, Alexander Sanga. Tafadhari wafanye hivyo ili kuepuka kutuvuruga,” alisema Dk Tiboroha.

Awali ilielezwa kwamba Stand imeachana na Chanongo ambaye alijiunga na timu hiyo baada ya kuwa ameng'ara Simba, lakini wakamtuhumu kwa utovu wa nidhamu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV