June 30, 2016


Yanga inatarajia kuanza mazoezi ndani ya siku mbili na kambi itakuwa kati ya Dar es Salaam au Mwanza.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema wachezaji wamepewa mapumziko ya siku mbili tu. Yanga inatarajia kuwavaa Medeama kutoka Ghana katika mechi itakayopigwa Julai 15.

“Baada ya hapo tunaanza mazoezi, halafu itakuwa ni kambi kwa ajili ya maandalizi ya mechi ijayo ya Kombe la Shirikisho.

“Kambi inatarajiwa kuwa hapa nyumbani, kama si Dar es Salaam basi itakuwa Mwanza. Lengo ni kupata utulivu kwa ajili ya maandalizi.”

Yanga inalazimika kufanya juu chini kuifunga Mo Bejaia ili kuamsha matumaini angalau ya kusonga nusu fainali.


Ugumu unatokana na vipigo mara mbili, ikianza kufungwa kwa bao 1-0 ikiwa ugenini dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria, halafu ikalala kwa idadi hiyo ikiwa nyumbani dhidi ya TP Mazembe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV