June 5, 2016

MAXIME

Uongozi wa Mtibwa Sugar umesita kulizungumzia suala la kutaka kumrejesha kikosini Salum Mayanga ambaye sasa anakinoa kikosi cha Prisons ya Mbeya.

Kumekuwa na taarifa kwamba Mtibwa Sugar imeamua kumrudisha Mayanga aliyewahi kuwa bosi wa kocha wa sasa wa Mtibwa, Mecky Maxime ambaye imeelezwa anapelekwa Kagera Sugar.

Mratibu wa Azam FC, Jamal Bayser ameiambia SALEHJEMBE kuwa, sasa wasingependa kulizungumzia suala hilo.

“Wewe umesikia wapi,” alihoji Bayser.

Alipoelezwa, kamwe huwa watoa habari hawatajwi, akasema:

“Nisingependa kulizungumzia suala hilo, kwanza sasa ni mapema sana.”


Imeelezwa kwamba Mtibwa Sugar wanataka kujiimarisha zaidi ili kuingia kwenye kundi la timu zinazowania ubingwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV